Rungu la Mulugo lawashukia wakuu wa shule saba

mulugo

RUNGU la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,  Philipo Mulugo limewashukia wakuu saba wa shule za msingi wilayani hapa kwa kupewa adhabu za kuteremshwa vyeo baada ya shule zao kujihusisha na udanganyifu kwenye mitihani.
Walimu hao ni wale ambao shule zao wanafunzi wake walibainika majibu yao kufanana katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika mwaka jana hivyo kusababisha kufutiwa matokeo ambao wanafunzi husika walipewa adhabu ya kurudia mitihani mwaka huu.

Naibu Waziri Mulugo alitoa agizo la walimu hao kuteremshwa vyeo kwa maofisa elimu wa halmashauri za wilaya na Mji wa Korogwe juzi, alipokuwa wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kikazi ambapo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa sekta ya elimu.

Walimu waliokumbwa na sakata hilo na shule wanazotoka kwenye mabano kwa upande wa halmashauri ya wilaya ni Karimu Awadhi (Hale), Eliakim Mbise (Kerenge), Ramadhani Kisairo (Rwengera Estate), Dastan Daudi (Pambei) na Mohamed Kombo (Vuluni).

Wengine ni Elisante Elibariki wa Shule ya Msingi Welei aliyehamishiwa Wilaya ya Kilindi ambaye hata hivyo imeelezwa kwamba tayari anatumikia adhabu hiyo ya kuteremshwa daraja huko aliko na Rashid Shekigenda wa Shule ya Msingi Antakaye Korogwe Mjini.

Katika mkutano na walimu wa eneo la Korogwe Mjini, Mulugo alielezea masikitiko yake juu ya hali ya ufaulu wa wanafunzi ambapo alisema ingawaje kimaandishi inaelezwa kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka lakini uhalisia hauelezi hivyo kwa mazingira yaliyopo.

Naibu Waziri Mulugo aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa toka kwa ofisa elimu wa halmashauri ya mji kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa wanafunzi wa darasa la saba, hapo aliweza kuzikumbuka baadhi ya shule zilizofutiwa matokeo kwa udanganyifu.

Baada ya naibu waziri huyo kuuliza swali hilo Ofisa Elimu, Maajabu Nkanyemka alijibu kuwa bado na kuitaja shule iliyofutiwa matokeo kuwa ni Antakaye ambapo mwalimu mkuu aliyekuwepo mkutanoni aliitwa mbele na waziri akiulizwa maswali kadhaa na baadaye na afisa elimu wa halmashauri hiyo ya mji alitakiwa kutekeleza agizo la kumteremsha cheo.

Kuhusu majibu juu ya suala la upungufu wa vitabu shuleni taarifa ambayo alisomewa, Mulugo aliwatoa hofu walimu kwamba serikali imetenga fedha za kutosha kukabili tatizo hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s