MBINU ZA KUFUNDISHA KISWAHILI

KISWAHILIBY PAUL MEELA

KITABU HICHI KIMEANDALIWA NA PAUL MEELA

LENGO:Kuuza na kuendeleza   Kiswahili Tanzania.
:Kuwasaidia  waalimu tarajali katika mafunzo yao ya ualimu

UMUHIMU WA MWALIMU KUANDAA SOMO:

 1.    Awae na uhakika na anachokifundisha
 2. Humsaidia Mwalimu kuandaa Zana.
 3. Humsaidia Mwalimu kuchagua Mbinu za kufundishia.
 4. Mwalimu hujiamini wakati anapofundisha.
 5. Mwalimu atatumia Muda Vizuri wakati wa kuwasilisha Somo.         MATATIZO:

 

  1. Mwalimu anaweza kutoka nje ya Somo.
  2. Anapoteza Muda mrefu.
  3. Anaweza akasababisha fujo na kelele Darasani.
  4. Kushindwa kujibu Maswali kwa Ufasaha.
  5. Mwalimu kushindwa kufikiri Malengo.
  6. Kutojua Zana za kufundisha.

                    AZIMIO LA KAZI:
Ni utaratibu wa utekelezaji wa Muhtasari ambao una mtiririko wa Mada zilizopangwa kwa mujibu wa Muda fulani.
UMUHIMU WA AZIMIO LA KAZI:

 

  1. Kuanda Andalio la Somo.
  2. Kuanda Zana.
  3. Kama Mwalimu amehama ni rahisi Mwalimu mwingine kuendelea.
  4. Kumsaidia Mwalimu kufanya Tathmini (Maoni)
  5. Kumsaidia Mwalimu kufundisha kwa Muda uliopangwa.

VIPENGELE VYA AZIMIO LA KAZI:
MWEZI,WIKI,KIPINDI,MADA KUU, MADA NDOGO,KAZI YA MWALIMU, KAZI YA MWANAFUNZI, VIFAA/ZANA,MAREJEO NA MAONI.
MFANO WA AZIMIO LA KAZI:

MWEZI WIKI KIPINDI MADAKUU MADA NDOGO KAZI YA MWALIMU KAZI YA MWANAFUNZI VIFAA REJEO MAONI
JANUARY 2 I Jua na Sayari Jua Mwalimu awaulize Wanafunzi nini Maana ya jua. Wanafunzi watashiriki kujibu nini Maana ya jua.
 1. Tochi.
 2. Tufe
   1. Chati ya Mfumo wa jua.
Kitabu cha Taasisi ya Elimu Darasa laSita,Atlasi. Somo limeeleweka vizuri.

ANDALIO LA SOMO
Ni Maelezo ya kimantiki anayoanda Mwalimu katika kuwasilisha Somo,pia ni utekelezaji wa Vipengele vilivyoko katika Azimio la Kazi.
UMUHIMU:

 1. Kusaidia kufundisha Somo kwa Muda unaotakiwa.
 2. Kusaidia kujua idadi ya Wanafunzi Darasani.
 3. Kusaidia kujua Vifaa na Mbinu atakayotumia.

Kusaidia kujiamini wakati anapofundisha.
MFANO WA ANDALIO LA SOMO:

TAREHE SOMO DARASA MUDA KIPINDI IDADI
WALIOSAJILIWA
IDADI
WALIOPO.
WAVU WAS
WAV WAS

MADA KUU.Kilimo cha Mazao ya Biashara.
MADA NDOGO.Kilimo cha Pamba.
MALENGO MAKUU.Kujua Mazao ya Biashara.
MALENGO MAHSUSI.Kujua nyanja ya kipindi cha pamba.
VITABU VY REJEA-Wafanya Kazi wa ulimwengu Darasa la Saba.

VIFAA VY KUFUNDISHIA-Mti wa Pamba,Pamba yenyewe,Mbegu.
MCHAKATO WA UFUNDISHAJI:
Mfano:

HATUA MUDA KAZI YA MWALIMU KAZI YA MWANAFUNZI TATHMINI MAONI
Utangulizi 05
Maarifa Mapya 15
Kukazia Maarifa 10
Kutumia Maarifa. 05
Hitimisho. 05

TATHMINI YA MWALIMU…………….
TAHTMINI YA MWANAFUNZI…………
MAONI…………..

JINSI YAKUTUMIA OMNESHO MBINU  KUFUNDISHA MSAMATI
Msamiati ni jumla ya maneno yana yotumiwa na watu katika lugha.

 1. mwl aandike msamiati ubaoni(agana)
 2. mwl aonyeshe tendo la kuagana
 3. mwl aulize nitendo gani anafanya
 4. wwanafunzi wonyeshe ishara ya kuagana
 5. wanafunzi watunga sentensi ya naeno kuagana
 6. wanafunzi waandike sentensi kwanye madaftari yao

NAMNA YA KUTUMIA MAELEZO KATIKA  KUFUNDISHA IMLA

 1. Namna ya kutumia  alama za maandishi
  mfano:,.:;//’-
 2. mwalimu asome mla wanafunzi wasiandike
 3. mwalimu asome wanafunzi waandike
 4. mwalimu asome kwa mara ya mwisho

STADI YA KUANDIKA
NAMNA YA KUFUNDISHA STADI YA KUANDIKA

 1. mwl michoro ya kuandika herufi mbalimbli
 2. kuandika herufi hizo ubaoni
 3. kuandika neno la herdufi hizo
 4. kuandika maneno mafupi

JINSI YA KUFUNDISHA DARASA LA PILI KUANDIKA KIFUNGU CHA HABARI

 1. Mwalimu aandika habari fupi ubaoni kwa hati ya wima
 2. wasome kwa sauti
 3. wanakili katika hati ya kuunga
 4. hati ya chapa darasa la kwanza na hati ya kuunga kwa darasa la  pili hadi la saba

JINSI YA KUFUNDISHA IMLA KWA DARASA LA KWANZA NA LAPILI
1 Mwalimu asome kifungu cha  imla chenye alama:-

 • mkato
 • nukta
 • ulizo

JINSI YA KUANDAA INSHA KWA DARAS LA  TAU  HADI LA SABA.
Maelezo
-vidokezo.
-utangulizi
– kiini
-mwisho
mfano
kilimo cha mtama
utangulizi-  nini maana ya matama.
-mtama mwenyewe
kiini-uutayarishaji w a samba
mwisho-\umuhimu wa mtama
AINA ZA INSHA

 1. Insha ya kuongozwa

Insha huru
JINSI YA KUTUMIA MBINU YAMAZUNGUMZO KUFUNDISHA UTUNGAJI WA  MAELEZO YA PICHA

 1. Mwl aandae picha za kutosha kufanya utungaji mfano:picha ya gari,mbuzi n.k
 2. mwl awagawie picha wanafunzi
 3. wanafunzi watoe maelezo kufhusu picha hizo mfano:hii ni picha ya nini?
 4. mwl aangalie matamshi sahihi ya wanafunzi

\SWALI

 1. Chora picha anuai zinazoonyesha shughuli zakila siku asubuhi hadi jioni
 2. kusanya picha mbalimbali katika magazeti zinazoweza kutumika katika somo la  utungaji

NAMNA YA KUTUMIA MBINU YAMAZUNGUMZO KUFUNDISHA  SOMO LA KITENDAWILI

 1. Maana ya kitendawili  ni tungo fupi zenye kudai jibu.
 2. mwl atoe mfano mmoja wa kitendawili
 3. wml achague wanafunzi watatu mmoja aulize kitendawili na wengine wajibu wakishindwa wmpe mji
 4. zawadi zamakpfi  zitolewe
 5. walimu awaache wnafunzi waulue vitendawil mbalimbali na kuvitegua

NAMNA YA KUTUMIA MBINU YA MASWLI NA MAJIBU
KUFUNDISHA MIUNDO
Muundo ni mpangilio kamili katika sentensi.
Zipo alama 2 za kufunsdisha muundo

 1. alama ya kwanza ni
 2. alama ya pilini  ………………………….

mwalimu aulize maswa li  mengi ili kupa ta miundo mingi na misamiati
mfano;

mwalimu ana………………….. pikaa chakula
mama ata……………. shule

JINSI YA KUFUNDISHA DAARASA LATANO KUJANDIKA BAARUA
1.Anuani ya anayeandika brua hiyo

 • salamu
 • kiini
 • mwisho

2.mwl aandike mfano ubaoni
3.wanafunzi waandike barua ya kirafiki
4.chache zisomwe ubaoni
5.mwalimu asahihishe
MBINU YA MAZUNGUMZO HUFUNDISHA MATUKIO  YA KUBUNI

 1. Mwl andae tukiola kubuni mfano:njaa,mafuriko n.k
 2. maana ya matukio ya kubuni
 3. mwl aeleze tuiol kubuni
 4. wanafunzi watoe matukio yakubuni

KUTUMIA NYIMBO KUFUNDISHA HERUFI

 1. mwlimu atunge wimbo
 2. wimbo uandikweubaoni
 3. mwl aimbe mara mbili
 4. wanafunzi wmfuatilizie mwali
 5. wote waimbe  wimbo kwa pamoja

ALAMA ZINAZOTUMIKA KATIKA UANDISHI

 1. Nukta .
 2. nukta mbili :
 3. mshangao !
 4. ulizo?
 5. mkato/
 6. semi  ”   “
 7. Ritifaa  ‘
 8. dukuduku …………
 9. nukta mkato;
 10. nk

RITIFAA ni kuonyesha nafasi ya herufi au namba  mfano:-1988=’88
N’sharudi=nimesharudi
matamshi ya herufimfano:-ngoma ya  ng’ombe
KUANDIKA HERUFI

 1. Maandike herufi hewani wanafunzi wafuatilize
 2. mwalimu aandaemichoro ya herufi hizo
 3. mwalimu aandike herufu hio na wanafuni wafanyemaoezi ya herufi hizo.

KUSOMA
Irabu na konsonati
MATATIZO YA KUFUNDISHA STADI YAUSOMA

 1. matamshi mabaya ya lugha ya mwanzo
 2. shule kukosa vitu halisi,kama picha n akadi za ubaoni
 3. idadii kubw ya wanafunzi darasani
 4. ni vigumu kutambua matatizo ya  wanafunzi
 5. ukosefu wa  chumba cha kuwaka zana kama kadi nk

JINSI YA KUFUNDISHA  SILABI NA MAANDISHI

 1. mwl aonyeshe kitu halisi
 2. atamke neno la kitu hico au picha hiyo
 3. mwaliu atumie kadi zenye silabi
 4. wanafunzi wasome maneno ubaoni kwenye kadi.

DARASA LA SIT KUSOMA

 1. Habari yenyewe
 2. maneno magumu
 3. kutunga mwaswali
 4. kujuibu maswali
 5. kuacha  zoezi
 6. kusahihi sha zoezi

STADI  ZA LUGHA
1.Stadi pokeo-kusikiliza-masikio
-kusoma-macho
2.Stadi toleo-kuzungumza-mdomo
-kusoma -macho
NJIA ZA KUFUNDISHA
mwanafunzi-mazingira-mwalimuj-maudhui-zana.
SWALI
Zana haina  umuhimu wowote kwa mwalimu na mwanafunzi.Jadili.
ZANA ZAKUFUNDISHIA
Ni vielelezo ambazo mwalimu anavitmia katika kuwasilisha somo lake darasani.
AINA ZA ZANA

 1. Zana zakuonekana mfano:-mazingira halisi
 2. zana zakusikiaka  mfano:-radio
 3. zana za kusikika na kuonekana mfano:-TV,computer na sinema

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDAA ZANA

 1. Ukubwa wa zana.
 2. Idadi ya wanafunzi.
 3. maudhui yaendane na zana.
 4. uwwezo wa mwalimu katika kuelezea mada.
 5. kutumia rangi ili zana ionekane vizuri.
 6. zana iwe nadhifu
 7. izingatie mahitaji

SIFA ZA MALENGO MAHSUSI

 1. Huonyesha muhusika.
 2. Badiliko la tabia
 3. kiwangvo cha utendaji.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s