Aliyefariki atokea ghafla

msalaba

MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha  Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu, juzi walifurika katika Kitongoji cha Mabulugu kumshuhudia mwanamke Ngulima Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani humo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.

Habari zaidi kutoka katika kitongoji hicho zinasema mwanamke huyo bado amefungiwa ndani ya nyumba yake akifanyiwa dawa za kienyeji ili arudie katika hali yake ya kawaida, kwani kwa sasa anaonekana kama zezeta.

“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa kuamkia leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana mlango…wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na usiku alipewa chakula akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa mwanamke huyo.

Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa kienyeji amekwisha kuja kwa ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze kurudia hali yake na kwamba amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka maiti kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alithibitisha tukio hilo, lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za kishirikina.

Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika eneo la tukio kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni jana, maiti ya mwanamke huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.

Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.

Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe Ngitu Masisanga na mama yake mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua ghafla juzi baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.

Alisema  cha ajabu ni kwamba wakati wamelala nyumbani kwa marehemu sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku marehemu alitokea akiwa uchi.

Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na kutazama picha hizo na kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo alichukua tochi iliyokuwa ikiwaka na kuizima.

Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya kukimbia nje tulimzuia yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio tukakimbilia nje, licha ya kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu ufunguke ila na yeye aweze kutoka nje, kuna mtu amefanya dawa za kienyeji ndio tunasubiri majibu.”

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkula,  Cymthia Mugussi  alielezea jinsi mgonjwa huyo alipopokelewa hospitalini hapo na kwamba baada ya kumchunguza walibaini kuwa na upungufu wa damu, lakini baada ya kuchukua vipimo na kabla ya majibu kutoka alifariki dunia.

Hata hivyo wananchi wakiwamo wana nzengo wa eneo hilo waliendea maiti na kuileta kijijini hapo, ambapo ilikuwa tayari imebadilika sana kwa kuvimba tumbo kama mtu mwenye mimba na usoni kuonekana kama mzee tofauti na awali marehemu alipokufa na kuhifadhiwa hospitalini hapo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwamo mwenyekiti wa kitongoji hicho Amos Mapema, na mwenyekiti wa wana zengo, wanaeleza tukio hilo kwamba ni la tatu kutokea kwa muda mfupi katika kitongoji hicho, ambapo watu wamekuwa wakifariki ghafla.

Aidha, kutokana na hali hiyo wananchi waliazimia kuwa sasa wanawake ndio wawe wanachimba kaburi wakiwatuhumu kuwa wao ndio wachawi.

Diwani waka ya Lamadi alisema kuwa hadi jana saa 6:00 mchana maiti ya mwanamke huyo ilikuwa haijazikwa na kwamba polisi walienda katika eneo la tukio, ili kuwaambia wananchi waizike katika eneo la serikali.

Aidha habari za kuaminika zinasema kuwa baadaye wanazengo walibeba maiti ya mwanamke huyo na kuipeleka katika nyumba ya mtuhumiwa huyo ambamo sasa inadaiwa kuwa imevimba sana na imeachama na mdomo uko wazi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s