AJALI YA BASI LA SABENA YAUA 17 TABORA

AJALI YA BASI LA SABENA YAUA 17 TABORA

kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Bw.Mohamed Mpinga
Watu 17 wamekufa papo hapo na wengine kadha kujeruhiwa katika ajali ya basi ya kampuni ya ya Sabena ya mkoani Tabora.
Ajali hiyo iliyotokea katika kata ya kitunda jana kufuatia gurudumu la mbele la basi la Sabena kupasuka na kuanguka porini kata ya itunda wilayani sikonge
Majeruhi 77 ambapo kati yao watano hali zao si nzuri na wamelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya sikonge .
Basi hilo lilianza safari yake kutokea jijini mwanza kuelekea mkoani mbeya.,waliokuwa katika ajali hiyo ni pamoja na askari polisi wilaya ya uyui aliyetambuliwa kwa jina moja la Heri
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa imetokea majira ya saa 1 na saa 2 usiku wakati basi hilo likitoka Tabora mjini kwenda Mbeya na kuwa hadi sasa RTO na kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora wamekwenda eneo la tukio ambalo ni umbali wa zaidi ya km 200 kutoka km kutoka Tabora mjini kuelekea Mbeya
kamanda Mpinga alisema kuwa idadi kamili ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni utata kutokana na taarifa tofauti zilizofika ofisini kwake ambapo taarifa za awali zilidai watu 13 ,taarifa nyingine zinadai watu 16 hivyo alidai taarifa sahihi zitatolewa baada ya RTO na kamanda wa polisi wa mkoa huo kurejea kutoka eneo la tukio.
Mtandao huu wa PAULMEELA BREAKING NEWS utakureta habari kamili
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s