KIJANA MUSHI

DSC06618
KIJANA MUSHI AKIWA AMEJIPUMZISHA UFUKWENI BAADA YA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU.

Advertisements

“KILIMO ADUI WA NJAA”:WEO LOLANGULU

DSC06591

Wananchi wa kata ya ilolangulu wameaswa kulima kwa bidii ili kuepuka tatizo la njaa hayo yamesemwa na kaimu mtendaji wa kijiji cha ilolangulu polycap wakati akiwa anaongea na wajumbe wa WDC katika ukumbi wa shule ya msingi ilolangulu aliongeza kusema kuwa wananchi walime mazao ya chakula kama mtama,mihogo na mahindi wakati huu wa mvua a za masika ,
mtendaji huyo aliwataka wananchi waachane na imani potofu kuwa chakula cha mtama kinaliwa na jamii ya wasukuma tu na wao hawatakiwi kula chakulahicho..Aliendelea kusema kuwa vijiji ambavyo havijapata mahindi ya msaada waendelee kuwa na subira kama yakifika watagawiwa.

DIWANI LOLANGULU ATOA TSH 9,000,000

DSC06635
alieko katika picha hapo juu ni kaimu mtendaji wa kata ya ilolangulu akishukuru wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata WDC kwa mahudhurio yao mazuri katika kikao cha kupokea fedha hizi ambapo kila kijiji kimetakiwa kuchangia tsh 125,000/=kwa ajili ya kujazia kiasi kilichopungua katika fedha hizi.
Wanachi wa kata ya ilolangulu wamemshukuru diwani wao said ntahondi kwa kutoa msaada wa tsh milioni tisa kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha sekondari ya ilolangulu.
diwani huyo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya uyui alitoa fedha hizo baada ya idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kuongezeka kila mwaka

Njombe, Iringa waponda matokeo darasa la saba

 

TEACHERBY PAUL MEELA

WANASIASA wa Mikoa ya Iringa na Njombe  wameponda matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa  na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa, kwa kusema kuwa Serikali inapika bomu la wasomi ambao hawatakuwa na tija kwa  taifa.

Wanasiasa hao walitoa kauli hiyo juzi  katika mkutano wa kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza katika muhula ujao wa masomo wa mwaka 2013 kwa kanda ya Iringa, uliofanyika mjini Njombe ambapo walielezewa kushangazwa kwao na Serikali kuchagua hata wanafunzi wenye ufaulu D kwenda sekondari.

Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alisema elimu ya Tanzania imekosa mwelekeo kutokana na mwaka huu Wizara ya Elimu kuchagua wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mpaka waliopata wastani wa alama ya asilimia 24 kwa kila somo, badala ya asilimia 44 ili kujaza nafasi katika shule za sekondari.

“Serikali inapika bomu la wasomi ambao hawatakuwa na manufaa kwa taifa, kwa sababu haiwezekani kuchagua mpaka mwanafunzi asiyekuwa na sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza ili kujaza nafasi, wasomi hawa ndio wale wanaopasua watu vichwa badala ya miguu,” alisema Msigwa.

Mchungaji Msigwa aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuacha kujitapa kwamba mwaka huu wanafunzi wamefanya vizuri ikilinganishwa na mwaka jana, wakati wamechukua mpaka wale waliofeli kujiunga na elimu ya sekondari na kuitaka Wizara ya  elimu na mafunzo ya Ufundi kueleza sababu ya  kushusha alama za ufaulu kwa  wanafunzi mwaka huu. Naye

Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikujombe (CCM) alisema haina maana kuona taifa linapeleka wanafunzi wengi sekondari wakati waliofaulu ni wachache.

“Mimi naona haina maana kujisifia kuwa tumefaulisha na kupeleka sekondari wanafunzi wengi wakati waliofaulu wachache, kama wamefaulu wanafunzi 100 tupeleke hao hao badala ya 200 ili kujaza shule,” alisema Filikujombe.

Filikunjombe alipendekeza wanafunzi ambao  wamepata wastani wa alama ya chini ya asilimia 70 kuachwa kabisa kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari,  badala ya kuwapeleka sekondari ili kwenda kujaza  vyumba vya madarasa wakati hawana sifa ya kujiunga na elimu hiyo.

 

MATOKEO DARASA LA SABA.

ANDAAA

MATOKEO YA MTIHANI WAKUMALIZA ELIMU YA MSINGI SHULE YA MSINGI ULIMAKAFU

Waliofanya=24   wav-15 was 09                waliofaulu=20 wav-12  was 8

S/N

JINA LA MWANAFUNZI

   
 1. 1.         
KAPEMBA MUSSA
 1. 2.         
KAOMBWE MASHAKA
 1. 3.         
MUHOZYA SAMWEL
 1. 4.         
MTEMWA SAMWELI
 1. 5.         
TATU HAMISI
 1. 6.         
MWAJUMA ATHUMAN
 1. 7.         
ALLY RAMADHAN
 1. 8.         
MWAMVUA ATHUMAN
 1. 9.         
NYANZOBE MAGANGA
 1. 10.      
ELIZABETH MSAFIRI
 1. 11.      
MAYUNGA ISEME
 1. 12.      
SAID ISSA
 1. 13.      
JAFARI SALUM
 1. 14.      
KULWA SAMLI
 1. 15.      
TAUSI MSOZA
 1. 16.      
MAULIDI JUMANNE
 1. 17.      
MALIETHA PAWA
 1. 18.      
ASHURA MASHAKA
 1. 19.      
SELEMANI NASIBU
 1. 20.      
HUSSEIN JUMA
   

Wanafunzi hawa watajiunga na shule ya sekondari Ilolangulu kidato cha kwanza 2013

By P.Meela

Matokeo Darasa la Saba hadharani

WANAFUNZI

BY  PAUL MEELA
SERIKALI imetangaza matokeo ya darasa la saba mwaka huu, huku takwimu za matokeo hayo zikionyesha kuwa zaidi ya nusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 ni wale waliopata asilimia 40 ya alama kwenda chini katika matokeo hayo.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa wananfunzi 294,833 sawa na asilimia asilimia 52.58  waliopata daraja ‘D’ wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Hao wanaungana na wenzao 265,873 waliopata madaraja ya A,B na C ambao ni sawa na asilimia 47.41. Kwa mujibu wa taratibu za mitihani ya darasa la saba, jumla ya alama zote ni 250 ambazo zimegawanywa katika madaraja matano ambayo ni A mpaka E.

Mchanganuo wa madaraja hayo ni alama 201 hadi 250 kwa daraja la A, alama 151 – 200 kwa daraja B, alama 101 hadi 150 kwa daraja C, alama 51 – 100 kwa daraja D na alama 0 – 50 kwa daraja E.

Waziri Kawambwa alisema wanafunzi 560,706 walichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kati ya 865,534 waliofanya mtihani huo wa siku mbili; Septemba 19 na 20 mwaka huu na kwamba mwaka huu wasichana wamefanya vizuri katika mtihani huo kuliko wavulana.

“Wasichana waliofaulu ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 ya  wanafunzi 560,706 wakati wavulana waliofaulu ni 279,246 sawa na asilimia 49.80,” alisema Kawambwa alipokuwa akitangaza matokeo hayo na kuongeza:

“Matokeo yanaonyesha kuwa jumla ya wahitimu 3,087 walipata daraja A, wakati 40,683 walipata daraja la B. Wanafunzi 222,103 walipata alama za daraja C wakati  526,397 walipata daraja D. Watahiniwa waliobaki 73,264 walipata E”.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013, imeongezeka kwa asilimia 8.8 ikilinganishwa na wanafunzi 515,187 waliochaguliwa mwaka jana.

“Mtihani wa mwaka huu, kwa mara ya kwanza watahiniwa walifanya kwa kutumia teknolojia mpya ya Optical Mark Reader (OMR) na ulisahihishwa kwa kutumia kompyuta,” alisema.

Alisema matokeo haya yanaonyesha alama ya juu kabisa ilikuwa 234 kati ya 250 kwa wasichana na wavulana.

Kabla ya matokeo, wasichana waliofanya mtihani walikuwa 456,082 sawa na asilimia 52.68 na wavulana ni 409,745 sawa na asilimia 47.32,” alisema Dk Kawambwa.

“Watahiniwa 29,012 sawa na asiliamia 3.24 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo na ugonjwa,” alisema.

Dk Kawambwa alisema, kati yao, ambao hawakufanya mtihani wasichana walikuwa 12,501 sawa na asilimia 2.67 na wavulana ni 16,511 sawa na asilimia 3.87.

Waziri huyo  alisema,  udanganyifu katika mitihani kwa mwaka huu umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana.

“Waliofutiwa matokeo mwaka huu ni watahiniwa 293 ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo yao kwa udanganyifu mwaka jana,” alisema Dk Kawambwa.

Hata hivyo, itakumbukwa serikali ilionya mwaka jana kuwa mwanafunzi atakayebainika kujiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Katika mkutano huo wa jana na Waandishi wa Habari, Dk Kawambwa hakutaja  viwango vya ufaulu kwa kila somo kama ambavyo imezoeleka katika mitihani iliyotangulia wala mkoa uliofanya vizuri au vibaya.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alipotangaza matokeo ya mwaka jana aliweka wazi viwango vya ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hisabati, ikilinganishwa na mwaka juzi.

Mulugo alisema viwango hivyo vilikuwa vimepanda kwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2010 ambavyo ni Kiingereza kutoka asilimia 36.47 hadi asilimia 46.70, Sayansi asilimia 61.33 kutoka asilimia 56.05 na Hesabu asilimia 39.36 kutoka asilimia 24.70.

Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo akizungumzia matokeo hayo jana alisema: “Hili janga, kwa sababu ukifanya uchambuzi wa haraka utabaini kuwa wanafunzi waliopata alama za daraja la A ni asilimia 0.35 tu”.

Lyimo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), alisema upo uwezekano mkubwa kukawa na idadi kubwa ya wanafunzi wasiojiweza waliochaguliwa kwenda Sekondari, hivyo akashauri iandaliwe program maalum ya kuwawezesha wanafunzi hao kumudu masomo ya kidato cha kwanza.

“Kama wanafunzi zaidi ya nusu waliochaguliwa kwenda sekondari ni wale wa daraja la D, hapo kuna kazi kubwa sana, tunaweza kuwa na mbumbubu wengi Sekondari kwahiyo nashauri Serikali iandae walau mpango wa wiki mbili kabla ya shule kufunguliwa ili kuwasaidia hawa watoto,”alisema.

Lyimo alisema ofisi yake itaendelea kufanya utafiti ili kubaini sababu za kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mtihani huo na kwamba itatoa taarifa baada ya kupata matokeo ya kitaalamu kuhusu suala hilo.

Mwalimu akutwa mtupu Shuleni Lindi

mkuu wa moa lindi                          mkuu wa mkoa wa lindi

by paul meela

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa

Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.

Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.

Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.